Motivation Corner

MOTIVATION CORNER

MOTIVATION CORNER

Madam Violet Konyani FOUNDER WOMEN POWER FOR DEVELOPMENT ORGANIZATION HESHIMU NDOTO YAKO, ITUNZE IKUE. Kila mtu Mungu amempa upekee wake, maono yake na ndoto yake. Yaani mimi siweze kulala nikaoteshwa maono ya @⁨Da Aiyana⁩ au maono ya @⁨Christina Bianchi⁩, kila mtu Mungu anampa kuota kulingana na kile ambacho Mungu anakihitaji kutoka kwake. Ninachokiamini mimi ni kwamba kila mtu anapambana kweli ili aweze kutembea kwenye njia yake. Kama kuna mtu amesimama anasubiri muujiza bila kujitafuta ni lazima kutakuwa kuna shida mahali. Mungu akufungue macho uone vyema kama siyo uone sawasawa. Na wale ambao tayari tunaziishi tujifunze kwamba zipo nyakati tutapita tena nyingine ni za maumivu makali sana lakini lazima tufike. Ndugu yangu mmoja huwa anasema mapito hayo badala yakulize, yakusanye yawe nguvu ya kukuongezea bidii. 📌Ndoto hupitia wakati wa ukimya. Huu ni wakati ambao nguvu zako zitakuwa hazilingani na matokeo unayoyapata. Wakati huu hutokea kwa sababu ni wakati wa mbegu kukusanya nguvu ya kuchipua. Ni kama vile wale wafanya mazoezi jamani huwezi kupungua siku moja kila siku unavyoongeza jitihada ndivyo ambavyo unazidi kukua. Au wewe ni mkulima mbegu ikiwa haijaota haimaanishi imekufa unatakiwa kuendelea kuitunza hata kama hakuna unachokiona kwa juu. Sasa wapendwa, hapa huwa hatuachi eti kwa sababu huoni kitu, huu ni wakati tu, unachotakiwa kufanya ni kuendelea mbele bila kuchoka. Ukiwa mtu wa kuchoka kwenye hii hatua ya kwanza tu nguvu zikiisha maana yake safari yako imeishia hapa, kitu ambacho hakikuwa nia wala matamanio yako. 📌Ndoto hupitia wakati ambao kila mtu hakuamini. Kuna wakati kila mtu anakuwa na mashaka na unachokifanya. Japokuwa wewe mwenyewe unaona unachokifanya kwa sababu wewe ndiye mwenye matamanio na ndiye unaijua safari yako na una uhakika huko mbele yapo mazuri zaidi. Utashangaa kila anayekuzunguka hakuamini. Kila mtu anasema lake. Kila mtu anashauri lake. Lakini wewe kila ukichekecha akili yako unabaki kuwashangaa kwani hawa ni vipofu au? Nasema hivi ndoto yako ikifika mahali kila mtu hakuelewi ndio wakati sahihi wa kufanya zaidi ili uendelee kumshangaza mwovu shetani. Mi sijui wewe unafanya nini ila ndio nakupa hizo hatua. Pima kwako ina apply vipi, songesha gurudumu lako kazi iendelee. 📌Ndoto huwa inapitia wakati wa kuchoka. Kuna wakati unafika nguvu ambazo ulikuwa nazo za kupambania ndoto yako hautakuwa nazo tena, itakuwa kama vile umepoteza hamasa ya kupambana. Yani kuna ule wakati unafika unasema natamani kama liwalo na liwe tu nimechoka. Unatamani kuanza kitu kingine, tena kinakujia kila saa. 🔖Ndugu yangu hatufanikiwi kwa sababu hatuna nguvu za kufanya. Tunafanikiwa kwa kujilazimisha kuendelea kufanya. Muendelezo ndio njia pekee ya mafanikio. Unaweza ukawa kwenye maumivu lakini kila ukipiga jicho mbele unasema lakini naiona kesho njema sana lakini mbona nguvu sina? Shetani amekaa pembeni anasema mbona huyu anachelewa kuacha. Hakikisha unasimamia jambo lako unaloliamini mpaka linafanikiwa. Wewe ndio uliyeanza na ulijua kwanini umeanza. Kupita pagumu ndio kujua kwenyewe na kujifunza zaidi. Leo ukitembea peku ukakanyaga msumari utakumbuka umuhimu wa kuvaa viatu. Nikutie moyo ndugu yangu, mimi sijui wewe uko wakati gani pambania chako bila kuchoka wala kukata tamaa. Mungu hajakupa karama yako kwa bahati mbaya. Amekutuma ufanye kazi. Ukirudi kwake ukampe majibu yake. Najua upo wakati tunapita kwenye magumu sana sana tu. Huo ugumu ndio ukuaji wenyewe. 📍Hatuwezi kuvuka kwenye changamoto kama hatujakubali kuwa zipo, akili yako lazima ikubali kuwa hiki ninachokifanya changamoto nitakutana nazo tu zisiwe kiwazo cha safari yangu. 📍Ukiona changamoto zimezidi usiwakimbie watu tafuta msaada uinuliwe, kumbuka unachokifanya chochote wapo watu wanakifanya, pia omba ushauri kwao ili uendelee mbele. Watu wazuri wapo na wako tayari kukusaidia usiue kitu kabla hujakipambania. Kuna wakati tunaweza kabisa kuwa na vitu vizuri lakini haviendi labda hatukuanza kwa wakati sahihi au hatukushirikisha watu sahihi. Lakini ni muhimu sana kuusikiliza moyo wako kila wakati, ukiwa na moto wa presha nyingi za watu huko nje unaweza jikuta umeshindwa kufanya kila kitu. 📍Hakikisha unaheshimu ndoto yako, unaitunza na inakua usikubali kufia njiani. Tengeneza misingi imara uweze kujiimaarisha zaidi. Tengeneza misuli ya ukomavu kutetea kilicho ndani yako. Hicho kiko ndani, ndio maana watu wa nje ni ngumu sana kukiona. Kulinda misingi ya mafanikio yetu wapendwa wangu ni muhimu mno. Changamoto yetu wengi ni kutaka mafanikio bila kuwa na misingi imara na matokeo yake tunapanda kwa muda mfupi tunatakata tamaa tunapoteza kila kitu. Kuna wakati bora uchukue muda mrefu kujenga misuli yako iwe imara kulingana na kazi yako kuliko kufanya kwa papara dunia ijue kumbe unajimaliza mwenyewe. Wazungu wanasema “your public value is the product of your private investment.” Kabla hujataka kuwa bora kuliko kila mtu nje, jitahidi kuwa bora kuliko kila mtu wakati hakuna anayekuona. Kufeli kupo lakini kufeli sio sababu ya kukufanya usiendelee. Mtu anaweza badilisha muelekeo na akatengeneza safari nzuri sana akiamua. Yapo mambo mengi yanaweza kutokea njiani na yakasababisha safari yako kuwa ngumu sana, badala ya kukaa pembeni na kuanza kulalamika jiulize ni kitu gani kingine naweza kufanya? Then fanya. Usikubali kuwa mtu wa kukaa kaa tu kisa ulifeli. Hapana kila siku akili yako iwe sharp kuhakikisha unaendelea mbele. 📍Huwezi kukuza ndoto yako ukiwa umekumbatia kila aina ya vitu, vingine ni vizito vitakuangusha. Kubali mengine yapotee wewe ukue. Hata kama ni watu sawa tu. Lazima tujue kila mtu akija kwenye maisha ana sababu. Kuna atakayekuja kukaa. Kuna atakayepita. Kuna atakayekuja kuongeza thamani halafu akaenda zake. Kuna wengine inabidi waondoke ili uanze kujitambua. Njia ya kuiishi ndoto ina mengi sana. Kelele zote hizi ni kutaka wewe usikate tamaa kwenye hatua yoyote ambayo upo sasa. Hata watu watakao kukataa, jua ipo faida kwenye kukataliwa pia. Na mara nyingi watu wetu wa karibu ndio wepesi kutukatisha tamaa kwa sababu wanatujua, wanajua madhaifu yetu. Usikubali, funga dirisha lako mtafaana mbele huko.

Read more
MOTIVATION CORNER

MOTIVATION CORNER

By Mariam Kisimbe Advocate/Conflict Resolution Consultant HEKIMA YA MAPOKEO Kwa kawaida neno mapokeo tumekuwa tukilisikia kutokea nyumba za ibada na hasa kanisani. Lakini kupokea kwenye jamii yetu ni neno ambalo limekuwa likitumika (kitenzi) kumaanisha kufanya jambo fulani ambalo limekuwa likifanyika huko nyuma na wakubwa au watangulizi hivyo limepokelewa kama lilivyo na linafanyika kama lilivyo bila kubadilisha wala kupunguza. Maana nyingine ya mapokeo na hasa ambayo tutaimaanisha hapa ni kupokea ambako kunahusisha kulikaribisha jambo au kitu na ukalipatia umuhimu wake unaostahili. Kupokea kwa maana ya kulikaribisha au kulikubali jambo fulani ndio mzizi wa somo letu la leo. Kupokea kwa maana ya somo hili ni kusikia, kusikiliza na kupitisha kwamba sasa hiki nilichoambiwa ni changu mimi au la! 📌Kwa nini somo hili? Tupo kwenye wakati ambao tunapokea taarifa nyingi sana kwa uharaka na kwa namna ambayo haina mpangilio maalumu. Tupo kwenye wakati ambao mtoa taarifa au kitu fulani hajali wala hana haja ya kujiuliza ninayemwambia yupo kwenye hali gani au atapokea vipi hizi taarifa? Zamani kidogo hivi mpaka miaka ya 90 mwanzoni ilikuwa ikitokea msiba anatumwa mtu aende mahali fulani kutoa taarifa na hakuwa anatumwa mtu tu bali yule mwenye uwezo wa kutulia na anayeweza kutoa taarifa kwa usahihi bila kuleta taharuki. Na haikuwa kirahisi hivyo, wakubwa walifikia hatua kwamba anachaguliwa mtu wa kumtuma kulingana na ukubwa wa msiba. Kama kafariki ghafla mtu mzima ambaye kwenye jamii anahitajika sana na ni mhimili wa walio wengi anatafutwa mtu mzima mwenye akili timamu ndio akatoe. Ikibidi watu wanaitwa bila kutoa taarifa ya msiba mpaka wakutane ndo wajue nini ni nini. Kwa upande mwingine, Mnafikiri zamani hapakuwa na watu wanatoka kwenye ndoa zao? Kwani hawakuwa wanafumaniwa na kufumaniana? Lakini taarifa inavyotoka ni kwa staha sana kiasi kwamba inaweza kulinda hadhi sio tu ya wahusika bali wale wanaopokea walikuwa wanalindwa pia. Kila mmoja anatakiwa kuwa daktari wa nafsi, roho na mwili wake. Lakini muhimu kwa leo tunakazania udaktari wa NAFSI yako. Maana nafsi ndio inayopokea hisia na inapokea taarifa nyingi sana. Wapendwa wangu sisi ni binadamu…Binadamu yeyote ni mbinafsi na angependa kujiridhisha mwenyewe kwanza. Kila kitu kizuri binadamu atataka kiwe chake kwanza kabla hakijaenda kwa wengine. Binadamu ni mbinafsi sana na ni asili hivyo hawezi kukuchujia wewe taarifa hata moja. Yeye atafanya kwa nafasi yake anavyoona ni sawa wewe unayepokea jiandae kumeza au kuitema. Kuna mwalimu mmoja alimpigia simu mzazi akimpatia taarifa ya wito wa haraka shule, akamwambia “Hello! Wewe ni Mama fulani? Jumatatu asubuhi njoo shuleni mwanao ni shoga!” Mzazi akauliza “ee mwanangu shoga?” Mwalimu akajibu “ndio anafanya mapenzi na wanafunzi na amewaharibu watoto wa watu wengi.” Sijui mnaiona hii taarifa??!! Mtoto ambaye ni mpole na mzazi wake hajawahi kumtilia hata shaka achilia kwenye hayo mambo, pia sio kijana wa mambo mengi.., taarifa zikaja mbili kwa wakati mmoja ‎1. Ni shoga 2. Anaharibu watoto wa watu. Mama wa watu akaanza kutetemeka anatamani aende shule muda huohuo! Hata amuulize huyo mwalimu wa nidhamu ni nini kinaendelea, mwalimu hapokei tena simu. Lakini si kulikuwa na namna nyingine ya kumuita? Ilikuwa na umhimu upi wa kuyasema yote hayo?? Na ujue ilikua ni Ijumaa asubuhi, mtoto sio wa kulala bweni anarudi nyumbani. Mama anajiuliza aongee naye? Lakini hana taarifa kamili. Je akiongea naye nusu nusu mtoto atajisikiaje? Wapendwa, hizi hali haziepukiki!! Kifanyike nini kwenye ulimwengu huu ambao mtu anaweza kukuambia chochote? Mtu hajui umekula mara ya mwisho lini anakutana na wewe pap, anakwambia punguza tumbo Mariam au umenenepa sana siku hizi. Au mbona umepungua sana yaani umepauka kuna usalama huko? Mtu hamjawahi kukutana miaka na miaka tangu utoto wenu leo mnakutana anakuuliza watoto hawajambo? Pengine unahangaika kwa waganga na waganguzi kutafuta watoto. Ndio kwanza talaka imetolewa majuzi unatafuta kupona mtu anakuuliza “Mr. hajambo? Ndoa imekupenda.” Kwanza kabisa kama binadamu jiandae tu, mtu anaweza kukuambia chochote kwa namna yoyote. Utulivu ni nguzo muhimu sana. Kuna mtu aliwahi kusema ukiwa mtulivu unaweza kulala na maiti hata siku 3 na maisha yakaendelea. Utulivu una ngazi tatu: 1. Kusikiliza 2. Kutafakari 3. Kupokea Tunaona kupokea ni hatua au ngazi ya 3 na ya mwisho. Ukiiweka mbele utaumia. Sasa kuelewa hapa turudi kwenye mapokeo ya kanisani wale wa Roma na Lutherani mnafahamu. Na ndio maana kwa kizungu kupokea wanaita CONFIRMATION. Si ndivyo keki za watoto siku ya kupokea zinavyoandikwa? Hakuna anayepokea bila kuthibitishwa kwamba anapokea anachokifahamu. Lazima usomeshwe kwanza, Uelewe unachoenda kupokea, kisha upokee. Maana yake ni nini? Hata taarifa ya msiba ikija sio lazima uibebe kwa namna ile tunabebaga. Dawa yake hii hapa; 1.Sikiliza tena kwa makini sana…, kama taarifa ni nusu hata jirani yako hatakiwi kusikia. 2.Tafakari kwa kina kwa nini taarifa ije kwako? Wajibu wako nini kwenye hiyo taarifa na utatimizaje huo wajibu kama upo? 3.Kisha pokea kwa ajili ya utekelezaji. Sio kila taarifa unatakiwa kuifanyia utekelezaji. Lakini ukipokea kabla hujatafakari lazima utajikuta unaifanyia utekelezaji ambapo lazima uchemshe tu. Lazima ufahamu mtoa taarifa ana kusudi gani na wewe kwanza. Tunaumizwa sana na vitu ambavyo hatukuchagua viwe hivyo au hatuna mamlaka ya kuchagua. Ni kosa kubwa sana. Wewe ambacho kinatakiwa kukuumiza na ukakipokea kwa namna hiyo ni kile ambacho umechagua na una mamlaka nacho au ulikuwa na mamlaka ya kufanya tofauti na vile. *Chagua aina ya changamoto zako* Tumepewa mamlaka ya kukanyaga nge na nyoka. Sio lazima kila kitu kiwe sehemu ya maisha yako. Habari ya msichana wako wa kazi kutembea na mumeo sio changamoto yako. Kwa sababu msichana wa kazi unamlipa wewe na vigezo vya kuwepo kazini vinajulikana sioni kama kuna mjadala pale ambapo mtu kavunja masharti ya mkataba. Una sababu ya kumsimulia aliyekuletea? Aliyezaa nje swali sio kwa nini umezaa nje maana mtoto alishazaliwa, bali ni kutafuta akili ya kuweka mipaka huyo aliyezaliwa hasiharibu usitawi wa walioko ndani. Nimeenda milembe juzi kati tunaambiwa vichaa wengi wa kike hivi karibuni ni sababu ya ndoa na mahusiano. Nikajiuliza sana sana. Na ndio maana unaweza kuja kwangu na jambo lako zito nikakupa jibu moja tu, “Hii changamoto sio yako unalazimisha tu ije kwako.” Usipambane kubeba stress za wenzako. Chambua kwamba hii ni yangu au ya wengine? Ukijua sio sehemu ya changamoto yako shika jembe ukalime. Badilisha mtazamo wako. Badala ya kukaa kwenye kupambania ulichosikia au kupewa taarifa zingatia kile unachoweza kudhibiti kwa sasa. Kimeondoka nini na kimebaki nini? Jiulize hilo swali wakati wa kutafakari. Hakuna kisichowezekana chini ya jua. Na hakuna changamoto ambayo haina utatuzi. Wakati unajimaliza kumbuka hiyo hali haiwezi kudumu maisha yako yote. Sema sasa utabaki nayo mpaka lini ni maamuzi yako tu. Unaweza kukubali mtu achukue vyote leo tena haraka haraka ili upate muda wa kutafuta vingine. Unaweza ukakubali kuwaondoa uliowapenda na kuwaamini haraka haraka kwenye maisha yako ili waje ambao wanakupenda pia haraka haraka. Unakubali kusamehe haraka sio kwamba ni ujinga au upumbavu bali unataka nafasi ya kufanya mambo mengine kwa haraka haraka na hauna nafasi ya kubeba sana. Sisi waislam mtu akifariki ni sharti asikae sana. Yaani kama inawezekana afe na kuzikwa palepale. Sio tu kwa ajili ya aliyefariki bali kuwapa nafasi hata wale ambao wanaomboleza. Sio watu siku 5 hawajazika wanasubiri kaka wa Marekani afike. Waliopo eneo la tukio wanalia mpaka wanatundikiwa drip maana wanaona mwili wa mpendwa wao hapo. Unakubali kuachilia sio sababu ni rahisi au hujaumia, bali unajifanyia usafi wa mahali pa kukaa baraka. Nafsi ikikaa na migogoro hakuna kinaweza kueleweka maana hata mbili utaiona ni nane. Mwisho, jikumbushe kuwa hali nyingi ni za muda na kwamba uwezekano wa kuzishinda unao wewe. Jaribu kuiona kwa mtazamo mpana. Jamani mbinu hizi zinaweza kusaidia katika kusitawisha utulivu, lakini zinaweza kuchukua muda sababu kuna kitu kinaitwa mazoea. Usisahau pia nafasi ya Mungu katika haya yote. Lakini lazima tuweke mizizi ambayo itasaidia kuleta mabadiliko chanya kwenye kila tunachofanya. La sivyo kazi tutafanya lakini tutakosa matokeo ambayo tulitarajia. Nawakumbusha kwamba kupokea kwa maana ya somo hili ni kusikia kusikiliza na kupitisha kwamba sasa hiki nilichoambiwa ni changu mimi.

Read more
MOTIVATIONAL CORNER

MOTIVATIONAL CORNER

Lango la Ndoto: Mungu husema nasi kupitia ndoto tunazoota! Ndoto ni nini? Ni maono unayopata wakati umelala! Maono haya unaweza kupata kutokana na vyanzo viwili; 1. Mungu 2. Matukio ya siku, mawazo, etc Focus yetu ya leo ni ndoto anazotupa Mungu kama channel ya yeye kuzungumza na sisi: Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali. Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani; Kwa andiko hilo, safe to say, so long as unaota NDOTO, Mungu alishasema na WEWE na anaendelea kusema na WEWE! Wale wanaosema hawajawahi kuisikia sauti ya MUNGU au Mungu hajawahi kuwasemesha,..well, kwa mujibu wa hilo andiko, MUNGU anasema na wewe!! Yes, *ndoto ni SAUTI ya Mungu kwetu binadamu!!* Hence, kupuuza ndoto unazoota ni kuipuuza sauti ya Mungu! Kwanini Mungu anasema na sisi kwenye ndoto? 1.Kutufunulia vitu mbalimbali kama maono ya maisha yetu, majibu ya maombi yetu na kutupa mafundisho. Ndipo huyafunua masikio ya watu, Na kuyatia muhuri mafundisho yao, 2.Kutuonya juu ya mambo tunayoyafanya i.e tabia zetu, mienendo yetu, maamuzi yetu, kiburi, hasira,etc. Ili amwondoe mtu katika makusudio yake, Na kumfichia mtu kiburi; 3.Kutukinga na majanga na kutupa ulinzi. Yeye huizuia nafsi yake isiende shimoni, Na uhai wake usiangamie kwa upanga. *NOTE Hata zile ndoto tunazozi-label kwamba zinatoka kwa shetani, huwa sio hivyobali Mungu mwenyewe anakupa glimpse ya kuona nini KINAENDELEA KWENYE ULIMWENGU WAKO WA ROHONI kuhusu wewe vs Mungu, na wewe vs Shetani, ili UCHUKUE HATUA kuruhusu au kutoruhusu YATOKEE kwenye ulimwengu wako wa mwili!! Ndio maana ndoto za hivyo zinakujaga na mshtuko au mahangaiko fulani (some level of discomfort) ili kututingisha tusichukulie poa! Yeye hutiwa adabu kwa maumivu kitandani mwake, Na kwa mashindano yaendeleayo daima mifupani mwake; Mfano; umeota umepata ajali mbaya, au kuna msiba nyumbani, au anything negativehiyo ni taarifa ya mikakati iliyopangwa kwenye ulimwengu wako wa Roho.., unaonyeshwa kabla haijatokea kwenye ulimwengu wako wa mwili ili uzuie mapema kwa MAOMBI, KUFUNGA NA KUTOA SADAKA (depending on the gravity of the situation)! Usikemee tu halafu ukaendelea na maisha yako! Take your time in the place of prayer! Omba hata siku nzima wakati unaendelea na michakato ya siku., mpaka upate AMANI moyoni au NENO LA MAARIFA ndipo utakapojua umeshinda!! Since ndoto ni sauti ya Mungu inayosema nasi, ni MUHIMU kuwa na *DIARY* (physical au kwenye simu) ya kuandika ndoto zako!! Kama kuna principle maishani mwangu iliyonipa manufaa makubwa katika kuijua, kuitii na kuiamini sauti ya Mungu, ni hii tabia ya kuandika ndoto zangu kila ninapoota., regardless niwe nimeielewa au la! Mungu anajibu maombi kupitia ndoto! Huonyesha njia kupitia ndoto!! Ukisubiri uisikie audible voice ya Mungu kila wakati, well, utakosa mengi na utachelewa kwenye kukamilisha vitu vingi!! Ukiota ndoto ukashtuka usingizini, record audio kwenye simu (kama umechoka kuandika), usiseme utaandika asubuhi kwa sababu unaweza ukasahau details muhimu asubuhi ikifika! Andika TAREHE na MUDA wa kila ndoto unayoiota!! BWANA akanijibu, akasema, *iandike njozi ukaifanye iwe wazi sana katika vibao*, ili aisomaye apate kuisoma kama maji. Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia. Then, MUHIMU kuliko yote OMBEA NDOTO UNAZOOTA! Kila detail uliyoiona kwenye ndoto iombee, haijalishi kama umeielewa au la! Mungu mwenyewe atakupa tafsiri yake in time! Unapoombea ndoto zako unaruhusu yale mema yatokee na kuzuia yale mabaya/maovu yasitokee. I always say, Every dream is a brick to your future, a light to your present & a memory of your past, honor them. ~Beatrice By Beatrice Semba, Mwanasheria na Meneja Miradi (Women Power for Development).

Read more